Daimond, Lavalava wamvuruga Mmarekani

Friday February 21 2020

Daimond, Lavalava wamvuruga Mmarekani,NYOTA ya wasanii kutoka kundi la WCB, Diamond Platnums ,Swizz Beats.,

 

By Thomas Ng'itu

NYOTA ya wasanii kutoka kundi la WCB, Diamond Platnums na Lavalava imezidi kung'ara baada ya nyimbo zao kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii na msanii wa Marekani anayetambulika kwa jina la Swizz Beats.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa msanii huyo aliamua kupost nyimbo za wasanii hao na kuonyesha kabisa kuvutiwa na mdundo uliopo ndani yake.

Swizz Beats aliandika "Napenda nguvu inayotumika pale linapokuja suala la mziki," aliandika huku akiwa ameweka wimbo wa Lavalava unaojulikana kwa jina la 'Wanga'.

Msanii huyo pia aliweka wimbo wa Diamond 'Wanaona Gere' na kuandika "Najihisi na mimi nipo upande huu, kaka yangu Simba kila siku nipo upande tofauti," .

Nyimbo hizo hivi sasa zimekuwa zikitamba mitandaoni pamoja na vituo vingi vya redio na runinga kutokana na ubora wa utayarishaji wa video pamoja na mashairi yaliyotumiwa.

Advertisement