Corona yampa mchongo Mr Blue

Muktasari:

"Plani B  kazi zitafanyika sana online ambako mashabiki zetu watakuwa wanapata kazi zetu huku. Ni changamoto ya Dunia, inagusa kila binadamu kwa sehemu yake,hapa ndipo panahitaji ubunifu ili mambo yaweze kwenda," amesema.

MSANII wa kizazi kipya, Mr Blue amesema ugonjwa wa corona unaleta changamoto ya corona kiuchumi hasa kwa wale shuguli zao zinategemea mikusanyiko.
Amesema imekuwa ngumu kwao kupata kazi kwa maana ya matamasha ambayo yanakuwa yanategemea mkusanyiko wa watu na fasta akatafuta mchongo wa kumuingizia fedha kipindi hiki.
"Plani B  kazi zitafanyika sana online ambako mashabiki zetu watakuwa wanapata kazi zetu huku. Ni changamoto ya Dunia, inagusa kila binadamu kwa sehemu yake,hapa ndipo panahitaji ubunifu ili mambo yaweze kwenda," amesema.
Mr Blue amesema nikipindi cha kumuomba Mungu aepushie mbali ugonjwa huo, ili watu warejee kusaka kipato cha kujikimu kimaisha.