Chuchu Hans : Atoboa ukweli ishu za Ray

Muktasari:

  • Aidha ,katika hatua nyingine Chuchu Hans ambaye anayewania tuzo ya mwigizaji bora wa kike kupitia Tuzo za Sinema Zetu (SZIFF) aliliambia Mwanaspoti jinsi walivyoanza mapenzi na Ray, kwani ilisababishwa na watu na wao wakaamua kufanya kweli

KATIKA kila kinachotokea kwa staa kuna mengi huwa yanazungumzwa, mfano mzuri ni baada ya msanii wa filamu Bongo, Chuchu Hans kudaiwa kuachiwa nyumba na mzazi mwenzake Vincent Kigosi ‘ Ray’,na kubaki yeye na mtoto.

Mwanaspoti limepata nafasi ya kuzungumza na Chuchu na hivi ndivyo anavyofunguka:

Chuchu: “Kwanza watu waelewe mimi sijawahi kuishi nyumba moja na Ray,Ray anaishi kwao mimi naishi kwangu kwenye nyumba ambayo Ray amenipangia kabla hata sijazaa nae

Sasa inakuwaje hayo maneno ya kuambiwa mimi nimeachiwa nyumba jamani? Vitu vingine watu wanaongea hawana hata uhakika navyo.

Na hata hivyo katika mitandao ya kijamii, kuna suala lipo na linadaiwa kuwa wawili hao wameachana na kubakia mtu na mzazi mwenzake ambao wanalea tu mtoto.

Aidha ,katika hatua nyingine Chuchu Hans ambaye anayewania tuzo ya mwigizaji bora wa kike kupitia Tuzo za Sinema Zetu (SZIFF) aliliambia Mwanaspoti jinsi walivyoanza mapenzi na Ray, kwani ilisababishwa na watu na wao wakaamua kufanya kweli.

“Unajau kuna vitu watu hawavielewi kabisa, kwanza mimi hadi kuwa na Ray kimapenzi, ni kutokana hisia za maneno ya watu, kiufupi watu ndio wamelazimisha na sisi tukaamua kufanya kweli

“Yaani tulikuwa tunakutana kwenye kazi tu na tulikuwa tunaheshimiana kama mtu na mfanyakazi wake na hakuna mtu aliyekuwa na matamanio ya mapenzi na mwenzie,lakini kuna vitu vilisababisha hadi tukakutana na Ray, kama watu kutuhisi kuwa sisi ni wapenzi hapo ndio tukaamua kufanya kweli sasa.

“Unajua, siwezi kuzungumzia habari za kuachana na Ray au kama tupo pamoja, kwani tayari watu wameshajisambazia habari ambazo kwa madai yao wao wenyewe, na hii ni kutokana na mimi kutoishi nyumba moja na Ray.

“Labda niseme tu kuwa, mimi tangu nimeanza uhusiano na Ray, sijawahi kukaa na Ray nyumba moja, yeye anaishi kwao mimi naishi kwangu nyumba ambayo amenipangishia, watu wanaumizwa na nini mimi kutoishi naye nyumba moja?”

Ishu ya kuongeza mtoto

“Kiukweli sifikirii kuongeza mtoto. Yaani inatosha kabisa, kwa sasa najipanga kwenye maisha kwa ajili ya watoto wangu, na ndio maana mipango yangu ya mwaka huu 2019 kufanya kazi kwa bidii kwani nilipumzika kwa ajili ya kulea.”

Ampa pongezi Ray

“Kiukweli ukiniambia nikwambie Ray ni mwanaume wa aina gani kwa mtoto wake, ninaweza kusema ukweli ni baba wa ukweli, yupo makini sana kwa mtoto wake na hii sijajua sababu ni kuwa na mtoto huyo huyo tu au laa, ila nampa pongezi kwa hilo anajitahidi sana.”

Hata hivyo Chuchu ametaja sababu ya mtoto wao kuwa staa, ni kutokana na Ray kuambiwa mgumba na baadhi ya watu na hata alivyobeba ujauzito Chuchu alikuwa anaambiwa mimba sio ya Ray. Lakini mtoto amekuja kuzaliwa kafanana na Ray na kuupata ustaa wa haraka.

Chuchu alifafanua maneno yanayosambaa kuwa amefanyiwa mambo kishirikina kwa kushindwa kuona na Ray hadi leo hii,kwani hayo mambo huwa anayasikia kwa watu, ila yeye anachoamini ni riziki haijafika na ikifika haitakuwa na kuchagua dini ikiwa wao wapo dini tofauti.