Benny Kinyaiya: Hata kama nimeoa mzee haiwahusu

Muktasari:

  • Mtangazaji Kinyaiya ameshindwa kuweka wazi kuwa amefunga ndoa au hajafunga ndoa na kuishia kusema watu hayawahusu hata kama kafunga ndoa na mwanamke aliyemzidi umri.

Dar es Salaam. Mtangazaji maarufu, Benny Kinyaiya leo Feb 20, 2018 amevunja ukimya akiwataka watu kuacha kuzungumzia maisha yake na suala la kuoa kwake.

Akizungumza na redio ya EFM katika kipindi cha Uhondo, Benny amesema hata kama kweli amefunga ndoa na mwanamke aliyemzidi umri watu hayawahusu hadi kufikia hatua ya kumshambulia mtandaoni.

Benny alisema anashangaa watu kuingilia maisha yake binafsi, sababu kama imetokea kweli au sio kweli, yeye ameamua kwa nafsi ya mapenzi yake kwani mapenzi hayatizami umri na hapaswi kupangiwa.

"Ngoja leo niwafungukie hawa watu vizabizabina waliopo katika mitandao, maana kazi yao wakiamka asubuhi hata mswaki hawapigi wanaongelea habari za watu kama wanauhakika nazo, sasa nawaambia hata kama mfano nimeoa mambo yangu hawayahusu, maana wanajifanya kumjua sana yule mwanamke kama wao ndio mama mzazi wao.

Aidha Benny ambaye hadi mwisho wa kipindi ameshindwa kuweka wazi kuwa kama amefunga ndoa kweli au hajafunga, alimuwakia mtu aliye muuliza swali la kuwa amefunga ndoa na mwanamke ambaye sio sahizi yake kwa sababu ya kufuata pesa na kulelewa ili awe na maisha mazuri.

"Kwanza elewa kwanza kuwa mimi siku zote sio Marioo ninaye penda kulelewa na mwanamke mwenye pesa, mimi ni mtafutaji na nimeanza kutafuta toka nimemaliza shule na kuanza kupiga kazi, kwa wanaonijua mimi niko vizuri siombi cha mtu, siombi kodi kwa mtu, sitembelei gari la mtu, yaani nina kila kitu cha mwanaume kijana alichokuwa nacho

"Nina biashara zangu, nyumba, gari, nashukuru nimevuka levo ya kusubiri nipewe na niwaambie tu mimi ni baba wa familia ya watoto wawili, ambao wa kiume ana umri wa miaka saba na wa kike anaumri wa miaka mitano, mama zao tofauti"

Hata hivyo Benny aliuzwa swali la wanaume wenye umri mdogo kuoa wanawake walio wazidi umri yeye kama yeye anachuliaje? ambapo alisikika akisema haya:

"Nafurahia sana ndoa za mwanaume kumzidiwa umri na mwanamke, yaani mie naona sawa tu na kawaida sana, tena ni nzuri zaidi na rahisi kuelewana, sio unaoa mwanamke kutwa kutaka kwenda club na sehemu zingine za starehe, sasa aliyenizidi umri hana muda huo zaidi ya kukupa mipango ya maisha,"alisikika Benny akisema.

Hivi karibuni katika mtandao wa kijamii, kuna picha zinatembea zikimuonyesha Benny akiwa katika ofisi moja  ya Serikali akionekana ameshika cheti na mwanamke na kudaiwa wamefunga ndoa.