Asha Baraka awachana wasanii wakubwa nchini

Wednesday August 28 2019

 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka amewatolea uvivu wasanii wakubwa walioshindwa kujitokeza katika mkutano wa wasanii na Mawaziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo na Viwanda na Biashara.

Mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere, Dar es Salaam unalenga kujadili namna ya kuunganisha Taasisi za Cosota, Basata na Bodi ya Filamu kuwa kitu kimoja.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Asha Baraka alisema ni mkutano wenye tija kwa wasanii, lakini ameshangazwa na baadhi ya wasanii wakubwa nchini kutoshiriki.

"Waache hizo, huu mkutano unamhusu kila msanii, lakini kuna wengine tena wakubwa tu hawapo katika mkutano huu, sio poa," alisema Asha Baraka.

Baadhi wamefika kwa upande wa filamu yupo Elizabeth Michael 'Lulu' Jakline Wolper, Simon Mwakifamba, Muhogo Mchungu.

Kwa upande wa dansi baadhi yao ni Muumin Mwinjuma, Juma Kakere, Jimmy Gola, Asha Baraka, King Dodoo, Badi Bakule, Mjusi Shemboza na wengine wengi

Advertisement

Aidha kwa upande wa bongo fleva baadhi yao ni P Funky, AY, Mwana FA, Nikki wa Pili na wengine

Advertisement