Anti afunguka ishu ya kutemwa na Iyobo

Thursday November 22 2018

 

By Rhobi Chacha

ACHANA na ishu ya Tamasha la Wasafi na Fiesta, ishu inayovuma kwa sasa kama radi huko kwenye mitandao ya kijamii ni couple ya mastaa wawili, Anti Ezekiel na dansa wa Wasafi Classic, Moses Iyobo.

Anti Ezekiel ni bonge la muigizaji akitamba kinoma kwenye tasnia ya Bongo Movie, akicheza filamu kibao ikiwemo Signature, Nampenda Mke Wangu, Mrembo Kikojozi, Madame, Maigizo, Chanuo na Mama na pia ni mzazi mwenzake na Iyobo.

Penzi la wawili hawa limekuwa gumzo hasa shughuli kubwa wanayopewa wanawake wanaojaribu kumzengea Iyobo kwani, Aunt huwa anakaba hadi kivuli unaambiwa.

Lakini, taarifa ambazo zinavuma kwa sasa ni kuwa wawili hawa hawako tena pamoja kama ilivyokuwa zamani kwani, hata yale mapicha picha yamepungua sana huko kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, Mwanaspoti limemnasa Anti Ezekiel na kupiga naye stori mbili tatu kuhusiana na hilo na mwenyewe akafunguka yote hapa.

Pia, amefunguka kuhusiana na ishu nzima ya mtoto wao, Cookie na mambo ambayo yanaweza kuchukua nafasi hapo baadaye. Mwanaspoti: Mambo vipi Aunt?

Aunt: Poa, mzima wewe?

Mwanaspoti: Niko poa, pole best nasikia mmeachana na Iyobo?

Aunt: Hata miye nasikia watu wanasema, lakini miye bado nipo na Iyobo wangu kama kawaida.

Mwanaspoti: Miezi michache iliyopita ulitumia ukurasa wako wa Instagram kumlalamikia mwanamke, ambaye ulidai anajigonga kwa Iyobo huku ukilalamika kuna mpango wa kuvuruga familia yako. Vipi imekaaje hiyo?

Aunt: Yaani imetokea tu ili kufikisha ujumbe, si unajua sina kawaida ya kuweka maisha yangu kwenye mitandao ya kijamii, lakini kwa hilo ilibidi nifanye tu.

Mwanaspoti: Kwani vipi Anti, ulishawahi kupigwa hata kofi na Iyobo?

Aunt: Sio kofi tu, huwa tunapigana kabisa lakini baadaye kila mmoja akigundua amefanya kosa na ilikuwa ni hasira basi, anajirudi tunaombana msamaha na maisha yanaendelea.

Mwanaspoti: Ulishawahi kumfumania Iyobo au yeye kukufumania na mtu mwingine?

Aunt: Nilishawahi kumfumania mara nyingi na yeye alishawahi kubamba meseji kwenye simu yangu, lakini inaonyesha labda mtu alikuwa ananipenda na nikampotezea na ishu kama hiyo ya kufumania ni lazima itokee hasa kwa sisi ambao tuna majina tayari.

Mwanaspoti: Mna mpango wa kuongeza mtoto mwingine?

Aunt: Ndiyo, mmoja lakini sio kwa sasa.

Mwanaspoti: Siku hizi umekuwa sio mtu wa skendo sana nini siri yako kubwa?

Aunt: Ni kujitambua tu na hasa ukiangalia nina familia sasa, hivyo muda mwingi nakuwa katika majukumu na yale maskendo yalikuwa ni utoto tu na sasa nimeacha.

Mwanaspoti: Ni kitu gani kabisa ulikipenda kwa Iyobo?

Aunt: Unajua napenda sana mwanaume asiyekuwa na kero, asiyependa kuzungumza sana yaani kiufupi sipendi gubu, sasa kwa Iyobo vitu hivyo hana.

Mwanaspoti: Siku ukimfumani Mose Iyobo utachukua uamuzi gani?

Aunt: Daah sijajua aise, maana maamuzi yangu huwa yanatokea wakati huo huo.

Mwanaspoti:Asante sana kwa ushirikiano

Aunt: Karibu tena.

Advertisement