AliKiba sasa ni baba Keyaan

Monday April 8 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam. Mwanamuziki Alikiba ametangaza jina la mtoto wa wake wa kike aliyezaliwa miezi miwili iliyopitwa kuwa anaitwa Keyaan.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Kiba aliposti video ya watoto wawili wa kike wakimpongeza kwa kupata mtoto wa kike ilikuwa Februari 28 mwaka huu na leo kupitia ukurasa wake huohuo ameonekana akiwa amembeba mtoto anamnywesha maziwa na kuandika jina la mtoto huyo.

Kiba ambaye ni mzazi mwenzake na Amina aliandika 'Alhamdulilah' Keyaan kitu ambacho kimewafanya mashabiki wengi wa msanii huyo kuomba kuonyeshwa sura ya mtoto huyo.

Picha hiyo ambayo ameiposti saa saba mchana hadi sasa imetazamwa na mashabiki zake 34,046 na kutolewa comment 1581 nyingi zikiwa ni za pongezi na wengine wakiomba kuonyeshwa sura ya mtoto huyo.

Advertisement