Diamond: Bila dresscode, utaishia getini harusi ya Esma

Muktasari:

Esma alifunga ndoa Juni 26 mwaka huu na mwanaume anayetambulika kwa jina la Yahya Msizwa ambapo juzi alifanyiwa maulid na leo ndio sherehe rasmi.

 

Diamond Platnumz ambaye ni kaka wa Esma, ametoa masharti magumu kwa waalikwa kwenye sherehe ya harusi ya dada yake huyo.

Sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika leo Agosti 1, 2020 katika viwanja vya gofu Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Akihojiwa na televisheni ya Wasafi, Diamond ambaye ni mmoja wa wanakamati katika sherehe hiyo amewataka waalikwa kuzingatia mavazi yaliyopangwa katika siku hiyo (dresscode).

Mavazi hayo kwa wanaume ni rangi ya maruni wakati kwa wanawake ni flash pinki.

“Lazima tuzingatie dresscode,mtu lazima kujiongeza, yaani kama kwa Zuchu mtu kaja na gauni jekundu mara nini,shughuli sio yako ndugu yangu  hii shughuli umealikwa fuata utaratibu na usipofuata utaratibu utaishia nje.

“Kwa sababu kiukweli waalikwa ni wengi na hapa tumejitahidi kwelikweli mtu ambaye anapata kadi kuwakilisha ina maana ni bahati na tumemuheshimu kweli kweli , nasisitiza dresscode kwa sisi wanaume tunavaa maruni na kwa wanawake wanavaa flass pink,watoto wa mjini wanaijua bana hamuwezi kuniangusha,”amesema.

Pia amewataka wageni waalikwa kuheshimu muda katika shughuli hiyo inayotarajiwa kuanza saa 10:00 jioni na kutaka kutosubiri mpaka Diamond aingie.

 

 

 

 

 

 

 

Mzee Yusuf kuachia wimbo wa kwanza leo

S. Mzee Yusufu alitangaza kuacha kuimba taarabu mwaka 2016 na kujikita katika shughuli za ualimu wa dini na kutoa dawa.

Nasra Aabdallah

Siku chache baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki, Msanii wa taarabu Mzee Yussuf natarajia kuachia wimbo wake wa kwanza leo.

Hii ni baada ya kuwa nje ya tasnia hiyo kwa takribani miaka minne ambapo mwaka 2016 alitangaza kuacha kuimba taarabu na kujikita katika shughuli za ualimu wa dini na kutoa dawa.

Hata hivyo Machi 12 mwaka huu aliwashtua wengi pale alipoandika kwenye ukurasa wake kwenye mtandao Instagram kuwa anarudi mjini na ataimba mpaka agalegale na wiki iliyopita alipohojiwa alifunguka kuwa anarudi rasmi kwenye muzik.

Anafanya hivyo akiwa katika maandalizi ya onyesho lake lililokuwa lifanyike jana sikuu ya Eid lakini lilisogezwa mbele kutokana na msiba wa Rais Mstaafu awamu ya tatu,Benjamin Mkapa ambalo sasa linatarajiwa kufanyika mkesha wa kuamkia sikukuu ya nanenane.

.Katika ukurasa wake ametangaza kuachia wimbo wake huo leo unaokwenda kwa jina Najilipua kwa kuandika ‘Najilipua itakuwa hapa masaa machache,”.

Hii inahitimisha safari yake ya kurudi kwenye muziki, kwa kuachia wimbo wa kwanza tangu alipoacha kuimba.