Zuchu, Harmonize hii hapa trendi mpya

INAWEZEKANA utoaji wa nyimbo nyingi kwa pamoja maarufu kama Extended Play ‘EP’ ni heshima kwa wasanii au hata kukuza wigo kuongeza kipato kwa kuuza nyimbo kupitia mitandao mbalimbali.

Miaka 15 nyuma, ni wasanii wachache waliokuwa na mfumo wa kuachia albamu, wengi wao waliona ni jambo lisilokuwa na umuhimu pengine hakukuwa na miondombinu rafiki ya kufanya hivyo, ikiwemo soko lenyewe.

Kipindi hicho wasanii walikuwa wanaachia ngoma moja moja tu, katika kila muda wanaoona ni sahihi kufanya hivyo, hata hivyo wengi wao hali hiyo ilionekana kutokuwa na manufaa mazuri sana.

Wasanii wachache walikuwa wakikomaa na kutoa albamu, miongoni mwao ni ‘Lady Jay Dee’ aliachia albamu ya ‘Machozi’ mwaka 2000, mpaka sasa ana albamu tano ikiwemo ya mwisho aliyoachia mwaka 2017.

Kuna tofaufi kubwa na wakati huu ambao, wasanii wanauza nyimbo zao kupitia mitandao mbalimbali, ikiwemo Deezer, BoomPlay, YouTube na Audiomark.

Hata hivyo, uwepo wa soko na ushindani wa kimziki umewafanya wasanii kuona kuna umuhimu mkubwa wa kuanza kutoa albamu na kiukweli wasanii wameamka kwa kaisi kikubwa na kuanza kufanya hivyo.

Pengine hilo limechangiwa hasa na mapinduzi makubwa ya Bongo Fleva yaliyofanywa na baadhi ya wasanii nchini kwa miaka ya hivi karibuni.

Makala hii inaangazia wakali wa Bongo Fleva, ambao wameachia albamu zao kwa mwaka huu na ushindani umeahamia kwenye mitandao hata hivyo wanafanya vizuri.

COUNTRY BOY

Rapa huyo mwenye miondoko ya ‘Trap’ aliachia albamu yake ya kwanza Januari mwaka huu, albamu hiyo yenye nyimbo 30 akiwa na wakali tofauti kama ‘Young Lunya’ na Kaligraph Jones.

Country Boy alizundua albamu hiyo Januari 3, mwaka huu, katika ukumbi wa ‘Maisha Club’ na kusindikizwa na baadhi ya wakali wa HipHop akiwemo Moni Centrozone na Motre The Future.

ZUCHU

Mrembo mbichi kabisa na binti wa Malkia wa Taarabu, Khadija Kopa, Zuchu ameachia albamu ya kwanza akiwa na WBC, ikiwa ni mwezi mmoja na wiki mbili tu tangu kutambulishwa na Lebo hiyo.

Zuchu ameachia Extended Play ‘EP’, mpaka sasa inashika namba moja kwenye ‘Boomplay’ ikiwa na nyimbo saba tu, Zuchu pia ana ujumla wafuasi milioni nane kwenye You Tube, kwa ujumla wa nyimbo zake.

HARMONIZE

Kuachia albamu ya ‘Afro East’ ni mafanikio makubwa kwa msanii hiyu kwani, hakuwahi kufanya hivyo akiwa na ‘WBC’ ameachia albamu hiyo yenye nyimbo 18, akiwa na wakali, Yemi Alade, Kaligraph Jones na Mr Blue.

Uzinduzi wake ulikuwa wa kibabe sana, kwenye ukumbi wa Mlimani City, ambapo wasanii, waigizaji na viongozi mbalimbali walihudhuria akiwemo Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

IBRAAH

Msanii huyo chipukizi na zao la ‘Konde Gang’ ameanza kuteka hisia za watu baada ya kuachia ‘EP’ yenye nyimbo tano, ambazo kwa ujumla wake zimesikilizwa kinoma kwenye ‘Boomplay’

‘EP’ hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Steps’ inafanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali, hata hivyo Harmonize hakubaki nyuma kwa kushiriki kwenye wimbo wa One Night Stand.

JUMA JUX

Mzee wa ‘African Boy’ ilikuwa shemeji ya ‘Mimi Mars’, Jux naye hajabaki nyuma kwenye orodha ya wasanii walioachia albamu na ‘Ep’. Mkali huyo wa kutupia ameachia ‘EP’ yenye nyimbo 18.

Humo ndani kuna wakali wa Bongo Fleva akiwemo Diamond Platnumz na mwamba wa Kaskazini Joh Makini, Jux anafanya vizuri na sana na nyimbo hizo