Mbona Maua Sama fresh tu

Friday April 13 2018

 

By RHOBI CHACHA

HUKO kwenye mitandao ya kijamii kuna watu wanachonga sana, sasa wameingia kwenye anga za staa wa kike, Maua Sama na kuambulia shombo la kutosha tu.

Iko hivi. Huko Instagram kuna wanaomchambua Maua wakidai kuwa, msanii huyo anafanya ngoma kali na zinabamba kinoma lakini sura yake haivutii.

Sasa mwenyewe kawasikia na kuamua kufunguka akisema, kamwe hawezi kujibizana na watu wamaomkashifu kwenye mitandao kuwa ana sura mbaya.

Maua anayetamba na ngoma ya ‘Nakuelewa’ amelieleza Jiachie kuwa sio kama hasikii kauli za baadhi ya mashabiki wasiompenda na mara nyingi wamekuwa wakimtag katika akaunti yake ya Instagram.

“Kiukweli niko poa na wala sichukii kuambiwa nina sura mbaya kwani, sio watu wote wanaoweza kukubali katika kazi yako au kwa jinsi ulivyo.

“Sijaanza kusikia leo tangu naanza muziki ninaambiwa hivyo na bado naendelea kudunda kama kawaida, nin

gekuwa nawafuatilia basi nisingefika hapa katika muziki, ninawapotezea kinoma,” amesema Maua Sama.

Mbali na kutamba na ngoma zake kibao, pia Maua amekuwa Queen na chorus katika Bongo Flava kwa kupiga chorus matata kwenye ngoma za Sielewi ya Mwana FA na Kiba 100 ya Roma na Stamina.