Masanja anogesha Sauti ya Busara

Saturday February 15 2020

 Masanja anogesha Sauti ya Busara,MSIMU wa 17  wa Tamasha la Sauti za Busara 2020 ,Masanja Mkandamizaji.,

 

By Rhobi Chacha,Zanzibar

MSIMU wa 17  wa Tamasha la Sauti za Busara 2020 juzi Alhamisi  ulizinduliwa rasmi visiwani hapa na moja ya wasanii waliopata bahati ya  kuwa mshehereshahi (MC)  Masanja Mkandamizaji.

Asikwambie mtu Masanja ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Mgaya anaijua kazi yake bana, aliweza kunogesha tamasha kwa kuweka mbwembwe zake za uchekeshaji huku akizungumza rafudhi ya kabila ya Kisukuma.

Masanja alikuwa kila akishuka mwanamuziki jukwaani, anapanda yeye na kuanza kuizungumzia kauli mbiu ya tamasha inayosema 'Paza Sauti, pinga unyanyasaji  wa kijinsia' huku akielezea unyanyasaji unavyoathiri tasnia ya muziki hasa wanawake.

Alikuwa anatumia neno la ‘wanawane’ kwa kutaka watu waliohudhuria kumsikiliza, pia kuzungumzia kwa masihara pindi mwanamuziki wa kike akitaka kutoka kimuziki asilimia kubwa wananyanyasika kwa kuombwa rushwa ya ngono.

Mbali na hiyo Masanja kabla hajapanda jukwaani usiku kutangaza, mchana alikuwa maeneo ya Ngome Kongwe linapofanyika tamasha hilo, kwa ajili ya kufanya ‘sound cheki’ , ambapo alizungukwa na watu huku wengine wakitaka kupiga nae picha na wengine kutaka wachekeshweakama walivyokuwa wanamuona kwenye kipindi chao cha Orijino Komedi akiwa na Vengu, Mpoki,  Joti, Mc Regan na Wakuvywanga.

Tamasha la Sauti za Busara 2020 lina vikundi  29 vya  wanamuziki  kutoka nchini mbalimbali barani Afrika ambalo vimeanza kutumbuiza toka Februari 13 mwaka huu linaendelea hadi 16 Februari.

Advertisement