TIMU ya vijana wasiozidi miaka 12 ya Mikadini Youth iliwakata kilimilimi majirani zao wa Coastal Kings kwa kuwafunga bao 1-0 kwenye mechi ya kujipima nguvu iliyofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Bomu.
Bao hilo pekee lilifungwa na Seif Salim. |
|
MTANZANIA aliyekuwa anaidakia Bandari FC, Ivo Mapunda ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi hiki cha usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu Kenya msimu huu. |
|
BEKI matata wa AFC Leopards, Jonas Nahimana Paco, amejiunga na kikosi cha timu ya Rwanda kitakachojipima nguvu na Congo Brazaville, leo Jumamosi. |
|
AFC Leopards imepiga kambi yake mjini Mumias katika Kaunti ya Kakamega, ikijiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya KPL. |
|
MAGWIJI wa soka nchini, Gor Mahia, wanaohaha kurejesha ubabe wao, leo Jumamosi wana kibarua cha kujaribu makucha watakayoyatumia katika mashindano ya Afrika kwa kuvaana na El Mereikh ya Sudan. |
|
TIMU ya taifa ya soka ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17, Jumamosi ijayo itakuwa na kibarua kigumu cha kuishinda Nigeria kwenye mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia. |