Benitez Katajirika kimasihara kwa kulipwa fidia

Muktasari:

Real Madrid na Atletico ni mahasimu wakubwa kwenye soka la Hispania, lakini wazazi wake Benitez kila mmoja anashabikia timu yake, wanandoa mahasimu hawa, sijui ilikuwaje wakati wa timu zao zilipokutana kwenye Madrid Derby.

BABA mmoja shabiki wa Atletico Madrid, Francesco alikutana na mama mmoja, shabiki wa Real Madrid, mrembo Rosario Maudes na kufanikiwa kupata mtoto wa kiume, ambaye hatujui kama amekuwa upande wa baba yake au mama yake kwenye ushabiki wa mpira.

Huyu ni Rafael Benitez na hii ilikuwa miaka 57 iliyopita.

Real Madrid na Atletico ni mahasimu wakubwa kwenye soka la Hispania, lakini wazazi wake Benitez kila mmoja anashabikia timu yake, wanandoa mahasimu hawa, sijui ilikuwaje wakati wa timu zao zilipokutana kwenye Madrid Derby.

Kupenda soka kulimfanya mtoto wao pia, Benitez kujiingiza katika mchezo huo na hatimaye kuwa mmoja wa makocha mahiri kabisa duniani, akipita kwenye klabu nyingi za maana kuliweka jina lake katika anga za juu kabisa.

Katika kufanya mambo yake kwenda vizuri, kwa sababu Benitez amezinoa timu England, Italia na Hispania, hivyo amefanya jitihada za kutosha na kuzungumza lugha za nchi hizo kwa ufasaha mkubwa.

Mpinzani wake mkubwa katika ulimwengu huu wa soka ni Mreno Jose Mourinho, ambapo wawili hao hawajawahi kupikika chungu kimoja.