Ni presha

Muktasari:

  • Hataki kumpoteza mchezaji wa kiwango na hadhi ya Schweinsteiger, bila kujali ni kwa kiasi gani msimu umekuwa mgumu kwake, katika kufikia mwafaka katika jambo hilo ni sawa na kuamua na hitimisho lake kuwa, haiwezekani.

KATIKA toleo lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, Kocha Pep Guardiola alikuwa akipata tabu kufanya uamuzi kuhusu mchezaji wake majeruhi, Schweinsteiger ambaye licha ya kuukubali uwezo wake lakini kitendo cha kuwa na majeraha ya hapa na pale kilimtatiza na kumuweka njia panda kocha huyo. Endelea…

Hataki kumpoteza mchezaji wa kiwango na hadhi ya Schweinsteiger, bila kujali ni kwa kiasi gani msimu umekuwa mgumu kwake, katika kufikia mwafaka katika jambo hilo ni sawa na kuamua na hitimisho lake kuwa, haiwezekani.

Hata hivyo, hiyo ndiyo kazi ya kocha, analipwa kwa kazi hiyo, anatakiwa achukue baadhi ya maamuzi ambayo wakati mwingine yanaweza kuwa si sahihi.

Alikuwa bado hajapanga kikosi chake cha kwanza kwa ajili ya mechi ya jioni, huku zikiwa zimebakia saa tisa kabla ya mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal.

Pep bado alikuwa akiitafakari mechi hiyo kwenye uwanja wake wa nyumbani, anapiga hesabu iwapo ampange Schweinsteiger au Lahm katikati ya viungo.

Kroos kidogo hali yake si nzuri lakini ukimwangalia usoni haonyeshi dalili zozote za kutokuwa tayari kuikosa mechi.

Hata hivyo, Pep bado ni mwenye mashaka, kichwani kwake anaendelea kuifanyia upembuzi timu yake: “Sina raha hadi nitakapojua nani anacheza, si suala la timu itakavyoshambulia, bali ni nani mtu muhimu wa kuifanya kazi hii.

“Ni jambo moja kuwa na wazo lililotulia la namna ya kucheza dhidi ya mpinzani wenu lakini ni jambo jingine tofuati kuteua wachezaji bora wa kulifanya hilo, hapo ndipo uamuzi wa msingi unapokuja.”

Ni saa sita mjini Munich, wachezaji walikuwa wameshafanya mazoezi ya asubuhi, walikuwa katika maandalizi ya kusikiliza mazungumzo ya pili na ya mwisho kabla ya mechi.

Haya ni aina ya mazungumzo ambayo yanaanika mbinu za timu pinzani na kufuatiwa na mapitio ya haraka haraka ya namna ya kushambulia, kukaba mipira ya kona na ile ya adhabu ndogo hasa zinazopigwa pembeni.

Hata hivyo, akili ya Pep bado inafikiria kikosi cha kwanza, ana matatizo ya hapa na pale, Kroos ambaye anaonekana hayuko vizuri licha ya kutokubaliana na hali hiyo pamoja na Schweinsteiger ambaye naye hayuko fiti kwa asilimia 100.

Yote hayo yanamfanya Pep awe na mashaka, wasaidizi wake katika benchi la ufundi wanamshauri awatumie wachezaji hao ambao wameifikisha timu mbali katika Ligi ya Mabingwa Ulya, waliompitisha katika kipindi kigumu pamoja na majanga yao ya kuwa majeruhi, wengi wao wana hasira ya kutoa adhabu ya msimu wa 2012/13. Mmoja kati ya wasaidizi hao nilipata bahati ya kunywa naye kahawa nje ya vyumba vya kubadilishia nguo na akaniambia, “Ushauri wangu ulikuwa ni kuwapa zawadi watu hawa ambao wametufikisha mbali kiasi hiki, hii ni kama fainali, yatakuwa ni mafanikio ya ukweli kufikia robo fainali huku tukiwa tumeshikamana na watu hawa, wote watakapokuwa fiti wataongeza ushindani katika timu.

“Kama tukitolewa hapo tutaona wiki chache zilizobaki kwenye msimu kuwa ni nyingi hasa.”

Hapo maana yake ni kwamba Rafinha atacheza beki ya kulia, huku Lahm na Kroos wakisimama viungo wawili wakabaji, lakini Pep akilini kwake anafikiria mambo mawili, jana alikuwa katika mtazamo wa kukubaliana na wasaidizi wake.

Ni mchana na kwa wakati fulani ilionekana kama alikuwa mwenye uhakika, “Uamuzi wa kwanza ilikuwa ni kuwatumia wachezaji ambao wametufikisha hapa, wachezaji ambao wanatakiwa kucheza zaidi na zaidi kutokana na aina ya majeraha waliyonayo.

Ni jambo la ajabu namna ambavyo kocha anabadili mawazo yake siku moja hadi nyingine, jana yake alikuwa wazi kabisa, mechi hii ina maana kubwa katika msimu wao, matokeo yatamaanisha ama kuwapa moja ya jukumu lao muhimu au kufikia hatua yao ya mwisho.

“Mechi ya kesho ni muhimu kwa sababu kwenye ligi tayari mambo mazuri kama tukitolewa kama tukitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa msimu wote utaharibika, ni lazima tufikia hatua ya robo fainali na baada ya hapo tuendelee na kazi.

Itaendelea Jumanne ijayo…