Mourinho kuwapanga Lukaku, Zlatan pamoja

Muktasari:

Kocha Jose Mourinho anataka kutumia mfumo wa 3-5-2 ili aweze kutumia washambuliaji wote wawili kwa pamoja.

London, England. Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na Romelu Lukaku watacheza pamoja katika safu ya ushambuliaji ya Manchester United.
Kocha Jose Mourinho anataka kutumia mfumo wa 3-5-2 ili aweze kutumia washambuliaji wote wawili kwa pamoja.
Jambo hilo linategemea kutoka kwa kuwaweka pamoja Lukaku na Ibra wakati Mswedi huyo atakapokuwa fiti.
Mourinho alisema: “Wachezaji bora wanacheza pamoja. Ni rahisi kwao kucheza pamoja. Msimu huu tumecheza mechi nyingi na washambuliaji wawili, hasa pale tunapocheza na mabeki wawili nyuma.
“Mabeki wapembeni wanaongeza mtu moja katikati hivyo ndivyo tunavyofanya, tumeshafanya hivyo na tulishajiandaa tangu mwanzo wa msimu.
Ibra aliweka wazi wiki hii anataka kucheza namba 10. Hakuna mtu ndani ya United wa kuzuia timu hiyo kwenda kwa mfumo wa 3-5-2 msimu huu, si Juan Mata wala Henrikh Mkhitaryan.
Mourinho alisema: “Ibra anauwezo wa kucheza kokote. Nimefurahi kwa sababu nimepata machaguo mengi, nashukuru kwa sababu timu itakuwa bora zaidi.
“Ninafuraha kwa sababu nitakuwa na wachezaji wengi wa kuwatumia, sitaki kufanya hali iwe ni  Zlatan na Romelu kwa sababu itakuwa ni Zlatan na Romelu.”