Xavi : Hispania yote hakuna kama Iniesta

Muktasari:

Kauli ya Xavi imekuja muda mfupi baada ya Iniesta kuaga Barcelona katika mchezo wao wa juzi usiku dhidi ya Real Sociedad.

Madrid, Hispania. Nyota wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez amesema, Andres Iniesta ni mchezaji wa aina yake aliyewahi kutokea nchini Hispania.

Kauli ya Xavi imekuja muda mfupi baada ya Iniesta kuaga Barcelona katika mchezo wao wa juzi usiku dhidi ya Real Sociedad.

Iniesta alibubujikwa na machozi alipoaga rasmi baada ya kucheza kwa mafanikio Barcelona ndani ya miaka 16.

“Huyu ni mchezaji wa aina yake kuwahi kutokea katika historia ya Hispania,” alisema Xavi aliyekuwa akicheza pacha na Iniesta katika safu ya kiungo kwa miaka 13.

Iniesta, aliyetwaa Ubingwa wa Ulaya na Dunia, ana rekodi ya kutwaa mataji 32 akiwa Barcelona aliyojiunga nayo tangu akiwa kinda.