Wenger awachenjia wakongwe kina Henry

Saturday September 9 2017

 

LONDON, ENGLAND. Arsene Wenger amevunja ukimya na kuamua kuwachenjia nyota wa Arsenal katika kikosi hicho akiwaambia hata wao hakuna aliyekuwa bora.

Mastaa wa zamani wa Arsenal; Ian Wright, Thierry Henry, Lee Dixon, Paul Merson na Martin Keown, wamekuwa wakiwashambulia kwa maneno makali wachezaji wa sasa wa timu hiyo wakiwashutumu kwa kucheza hovyo.

Wenger alisema: “Siku zote nimekuwa na tatizo la kuelewa kinachosemwa na hawa magwiji. Nilikuwa na wachezaji wote hao, nao walikuwa na udhaifu wao kama ilivyo kwa wengine.