Wenger atoa maagizo mazito kwa wachezaji

Muktasari:

Wenger aliwasihi wachezaji wake kuzingatia ustaarabu wanapokuwa wameshinda au wamefungwa ili kuimarisha nidhani ndani na nje ya uwanja.

England. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amewatahadharisha wachezaji wake kuepuka kufanya vurugu iwapo inapotokea wamefungwa au wakishinda.
Wenger aliwasihi wachezaji wake kuzingatia ustaarabu wanapokuwa wameshinda au wamefungwa ili kuimarisha nidhani ndani na nje ya uwanja.
Kocha huyo Mfaransa aliwataka wachezaji wake kuwa kama wachezaji wa mielekea ili kuepuka jazba kwa wachezaji kama ilivyotokea kwenye mechi ya watani Manchester City na Manchester United.
Kocha huyo alisisitiza kwamba wachezaji wanapaswa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, hata kama wameshinda au wamefunga.
Arsenal ndiyo timu pekee ya England ambayo inawakilisha katika Ligi ya Europa.