Wenger aamua kufungua makucha ya usajili

Muktasari:

Kuondoka kwa wachezaji Alexis Sanchez, Theo Walcott na Francis Coquelin kumemwongezea hasira Kocha Wenger na kuamua kuvunja ukimya.

England. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema anatarajia klabu yake itasajili wachezaji wengine ndani ya mwezi huu kabla ya dirisha dogo halijafungwa.
Kuondoka kwa wachezaji Alexis Sanchez, Theo Walcott na Francis Coquelin kumemwongezea hasira Kocha Wenger na kuamua kuvunja ukimya.
Wenger aliwahakikishia mashabiki wa timu hiyo kwamba kuondoka kwa Sanchez na kuingia Henrick Mkjitaryan kwenye dimba la Emirates, watarajie majina makubwa zaidi kutua kwenye klabu  hiyo ya Kaskazini mwa London.
Akizungumza ana gazeti la Metro kuhusu kuhama na kuingia wachezaji alisema,  “Siyo klabu yetu pekee inayondokewa na wachezaji, kwa kuwa bado tupo kwenye dirisha la usajili tutajitahidi kuleta wachezaji wapya na wenye majina makubwa duniani.”
Harakati za Wenger kutaka kumSajili mchezaji wa Borrusia Dortmund,  Pierre-Emerick Aubameyang ni kujaribu kupoza majeraha ya kuondokewa na Sanchez.