Viungo wote Man United wakali

Muktasari:

Mpango huo wa kunasa kiungo wa kati umedaiwa hauhusiani kabisa na hatima ya Paul Pogba hasa baada ya Kocha Jose Mourinho kuhitaji kuendelea kuwa na huduma ya staa huyo wa Ufaransa ili kikosi chake kiwe na uwezo wa kumiliki mpira na kupangua ngome ngumu za wapinzani.

MANCHESTER United wapo siriazi katika mpango wao wa kusajili kiungo wa kati katika dirisha lijalo la uhamisho wa wachezaji kwenye majira ya kiangazi.

Mpango huo wa kunasa kiungo wa kati umedaiwa hauhusiani kabisa na hatima ya Paul Pogba hasa baada ya Kocha Jose Mourinho kuhitaji kuendelea kuwa na huduma ya staa huyo wa Ufaransa ili kikosi chake kiwe na uwezo wa kumiliki mpira na kupangua ngome ngumu za wapinzani.

Staa wa Real Madrid na Ujerumani, Toni Kroos ndiye anashika namba moja kwenye ile orodha inayosakwa na Mourinho, lakini wasiwasi mkubwa uliopo ni kama Los Blancos watakubali kumpiga bei staa huyo.

Kutokana na hilo, Mourinho ameweka bayana orodha ya viungo wengine wakati anaotaka kusajili kama atakwama kwenye mpango wake wa kumnyakua Kroos.

Viungo anaowataka Mourinho kwenye orodha yake, yupo staa wa Napoli, Jorginho, kiungo Fred wa Shakhtar Donetsk’s Fred, Julian Weigl wa Borussia Dortmund na Carlos Soler wa Valencia.

Yeyote kati ya viungo hao ataifanya Man United kuwa na ufundi mwingi katikati ya kiwango na ndiyo maana Mourinho anahaha usiku na mchana kupata huduma zao na hilo linaweza kuwezekana kutokana na pesa ndefu waliyonayo.