United, Spurs zaanza mazungumzo ya Toby

MANCHESTER United imeanza mazungumzo na Tottenham Hotspur kwa ajili ya kumchukua beki mahiri wa kati wa timu hiyo, Toby Alderweireld, ambaye anaweza kuondoka katika dirisha hili la uhamisho baada ya kugoma kusaini mkataba mpya.

Hata hivyo, staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hataondoka kwa bei rahisi kwa sababu Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, anataka kiasi cha Pauni 75 milioni kwa ajili ya kumruhusu Toby kuondoka klabuni hapo.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, anasaka beki wa kukitia nguvu kikosi chake wakati huu akiwa hawaamini mabeki, Phil Jones na Chris Smalling na jicho lake limeangukia kwa Tobu ambaye licha ya mkataba wake kutarajiwa kumalizika mwaka 2020, lakini anaruhusiwa kuondoka dirisha hili kama kutakuwa na dili tamu.