Umeyasikia ya Pogba na Mourinho?

Muktasari:

Machester United itakuwa ugenini nchini Hispania kumenyana na Sevilla katika mchezo unaotarajiwa kuwa na msisimko.

London, England. Jose Mourinho amethibitisha kiungo mshambuliaji Paul Pogba atacheza mchezo wa leo usiku dhidi ya Sevilla.

Machester United itakuwa ugenini nchini Hispania kumenyana na Sevilla katika mchezo unaotarajiwa kuwa na msisimko.

Mourinho alisema Pogba atacheza mchezo huo baada ya jana kufanya mazoezi akionyesha kiwango bora.

“Linapokuja suala la mchezaji gani atacheza, sina tabia ya kuangalia umri au mshahara wa mtu,” alisema Mourinho.

Kauli hiyo itakuwa imeondoa sintofahamu baada ya kuibuka tetesi kuwa wawili hao hawaivi chunga kimoja katika siku za hivi karibuni.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, alikosa mchezo uliopita wa Kombe la FA dhidi ya Huddersfild kwa kuwa hakuwa na afya njema.

Kukosekana kwake katika mchezo huo kuliibua maswali mengi, lakini Mourinho aliwajibu wapinzani wake akidai hawezi kumzungumzia mchezaji mwenye miaka 24 ikiwa ni dongo kwa Pogba.