Ubingwa si kigezo: Conte aweka rekodi mpya England

Muktasari:

Kocha huyo amekuwa wa sita kufungashiwa virago katika misimu nane, kuanzia mjsimu wa 2009/10 wa kwanza alikua Carlo Ancelotti, Roberto Mancini, Jose Mourinho, Claudio Ranieri na sasa Conte.

London, England. Kocha Antonio Conte, ameongeza idadi ya makocha walioipa ubingwa Chelsea na kutimkuliwa msimu uliofuata baada ya kushindwa kurudia mafanikio.
Kocha huyo amekuwa wa sita kufungashiwa virago katika misimu nane, kuanzia mjsimu wa 2009/10 wa kwanza alikua Carlo Ancelotti, Roberto Mancini, Jose Mourinho, Claudio Ranieri na sasa Conte.
Ilipendaza kama wangekaa kama Alex Ferguson, ambaye alistaafu kwa heshima baada ya kukaa Old Trafford miaka 25 na kuipa Ubingwa wa mwisho msimu wa 2010-11, Manuel Pellegrini aliipa Manchester City ubingwa wa 2013-14 na kutimuliwa.
Tangu bilionea Roman Abramovich ainunue Chelsea mwaka 2003 ameshabadili makocha 11 na nin saba tu kati yao waliotwaa mataji.
Bilionea huyo kutoka Russia, anaokena haelewi chochote kuhusu neon uvumilivu katika medani ya soka.