Timu ya Ligi Kuu Uholanzi yatoa zawadi Bongo

Muktasari:

Eefke Hagen na  Emma van de Velde ni walimu  ambao wakati wanakuja nchini waliamua kupitia kwenye timu hiyo na kupewa zawadi hizo.

Arusha. Timu ya Heerenveen ya Ligi Kuu nchini Uholanzi maarufu kama Eredivisie imetoa zawadi ya jezi na viatu kwenye Kituo cha Future Star's kilichopo jijini hapa.
Eefke Hagen na  Emma van de Velde ni walimu  ambao wakati wanakuja nchini waliamua kupitia kwenye timu hiyo na kupewa zawadi hizo.
"Tuliwapa maelezo kidogo kuhusu Future  Stars na ndiyo maana hawakuona tatizo kutupa zawadi hizo chache kuwaletea, zitawasaidia," alisema Emma.
Future ni kituo cha kulelea vipaji vya soka kilichopo chini ya kocha mkuu, Afred Itael ambaye  anasaidiwa na makocha wengine.