Sterling aitolea mbavuni Arsenal

Muktasari:

Winga huyo mwenye miaka 22, alikuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Emirates akiwa ni sehemu ya kukamilisha uhamisho wa Alexis Sanchez kwenda Etihad.

London, England. Winga wa Manchester City, Raheem Sterling ametoboa siri kuwa hakuwai kuwa na mpango wa kujiunga na  Arsenal katika dirisha la usajili lililopita.
Winga huyo mwenye miaka 22, alikuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Emirates akiwa ni sehemu ya kukamilisha uhamisho wa Alexis Sanchez kwenda Etihad.
Kocha Arsene Wenger alikuwa akiangalia uwezekano wa kumnasa nyota huyo wa zamani wa Liverpool, lakini Pep Guardiola alikataa kumwachia nyota huyo wa England.
Kukiwa hakuna uwezekano wa kufanyika biashara yoyote kwa sasa, City imetangaza dau la pauni 60 milioni kwa ajili ya nyota wa Chile, ambayo ilikataliwa.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Napoli, Sterling hatilii maanani uvumi unaotolewa na vyombo vya habari.
Alisema: "Sihataji kuzungumza na kocha wangu (Guardiola), kwa sababu tayari tulishazungumza naye mwanzo wa msimu huu.
"Sina jambo baya lolote au hisia yoyote mbaya juu ya hilo.
"Niliamka siku mmoja nikiwa na kikosi cha England na kuona jambo hilo, sikuamini maneno hayo hadi nitakapoambiwa na kocha wangu baada ya hapo nitaamini.
"Si jambo ninalonitia shaka kwa sababu Pep ni mtu muawazi, angezungumza na mimi kabla ya hapo.
"Kwa hiyo sina sababu ya kuwa na hofu, na wala sifikiri jambo hilo hata kwa dakika moja."