Slimani awazamisha wachovu Liverpool

Muktasari:

Kipigo hicho kilikuja kipindi cha pili baada ya Liverpool kutawala mchezo ndani ya kipindi cha kwanza ikiwa kiungo wake mshambuliaji, Philippe Coutinho ambaye hata hivyo alitolewa na kuingia Benjamin Woodburn mara tu baada ya kipindi cha pili kuanza katika dakika ya 46.

SHUTI kali la mshambuliaji wa Leicester City, Mualgeria Islam Slimani la dakika ya 78, liliwaondoa wachovu Liverpool kwenye michuano ya Kombe la Carabao Cup (Kombe la EFL) kwenye Uwanja wa King Power.
Kipigo hicho kilikuja kipindi cha pili baada ya Liverpool kutawala mchezo ndani ya kipindi cha kwanza ikiwa kiungo wake mshambuliaji, Philippe Coutinho ambaye hata hivyo alitolewa na kuingia Benjamin Woodburn mara tu baada ya kipindi cha pili kuanza katika dakika ya 46.
Baada ya kushindwa kufunga huku kiungo mpya wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain na mshambuliaji Dominic Solanke wakipoteza nafasi za kufunga, moto ulianza kuiwakia Liverpool baada ya kuingia kwa OKazaki na kutupia la kwanza dakika ya 65 akimalizia basi nzuri ya Vicente Iborra na kuwaacha hoi Majogoo hao wa Liverpool, huku Leicester ikisonga katika raundi ya nne ya michuano hiyo.
Katika mechi nyingine za jana, Kocha Roy Hodgson alipata ushindi wake wa kwanza kama kocha wa Crystal Palace baada ya kuichapa Huddersfield bao 1-0, huku timu ndogo ya Bristol City ikiishangaza timu ya Ligi Kuu Stock City baada ya kuichapa mabao 2-0.
Huko Wembley, iliichukua dakika 65 Tottenham kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Barnsley huku Leeds ilisubiria hadi mipigo ya penalti kuamua ushidi wao dhidi ya Barnsley baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika dakika 90 katika Uwanja wa Turf Moor.
Joshua King alifunga katika dakika ya 99 ikiwa ni muda wa niongeza kuivusha Bournemouth raundi inayofuata baada ya kuifunga Brighton bao 1-0,  Middlesbrough ikiiondoa Aston Villa kwa kuichapa mabao 2-0, huku Swansea ikiiondoa Readind kwa kuichapa 2-0 nyumbani kwao.