Nahodha wa Manchester City kubaki Etihad hadi 2020

Wednesday October 11 2017

 

London, England. Manchester City inatarajia kumpa mkataba mpya mshambuliaji, David Silva ambao utamalizika mwaka 2020.
Hatua hiyo imetokana na mazungumzo ya muda yaliyokuwa yakiendelea baina ya klabu hiyo na mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania.
Mazungumzo baina ya pade hizo yanaonekana kuzaa matunda na Silva anatarajia kupata nyongeza ya mshahara hadi kufikia Pauni 150,000 kwa wiki.
Pep Guardiola amevutiwa na kiwango cha Silva tangu aliporejea uwanjani akitokea katika maumivu, lakini msimu huu amekuwa kwenye kiwango kizuri.
Silva kwa sasa ndiye nahodha wa Man City akivaa kitambaa cha beki wa kimataifa wa Ubelgiji Vincent Kompany ambaye ni majeruhi wa muda mrefu.
Mhispania huyo amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho tangu alipotia saini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo miaka saba iliyopita kutoka Valencia.