Man United yamfungia mlango Ronaldo

Muktasari:

Usajili wa mshambuliaji Mchile utamaliza uwezekano wa Ronaldo kurejea Man Utd

Madrid, Hispania. Ni suala la muda tu kabla ya Manchester United kutangaza kukamilisha usajili wa Alexis Sanchez kutoka Arsenal baada  ya kukubaliana na  Gunners kuwapa Henrikh Mkhitaryan ikiwa sehemu ya uhamisho huo.
Kuwasili kwa mshambuliaji huyo wa Chile kutamaliza mpango wa Cristiano Ronaldo kurejea Old Trafford, baada ya kuwepo kwa tetesi miezi iliyopita, lakini Jose Mourinho ameonyesha hana mpango wa suala hilo.
Alexis amekamilisha safu yake imara ya ushambuliaji wakiwa na wachezaji Marcus Rashford, Juan Mata, Romelu Lukaku, Anthony Martial, Jesse Lingard na Zlatan Ibrahimovic.
Hakutakuwa na usajili mpya kwa Man United mwezi huu na mwisho wa msimu huu malengo yao yatakuwa ni kupata kiungo mkabaji pamoja na beki.
Katika moja ya sababu za Ronaldo kutorudi Man United kwamba miamba hiyo ya England jezi namba 7, tayari imeshapata mtu mwingine.
Mourinho pia hana mpango wa kumsajili Gareth Bale ambaye msimu uliopita alionyesha nia ya kumtaka nyota huyo.
Sababu kubwa ya kumpotezea Bale ni hali yake ya kuwa majeruhi ya muda mrefu hivyo uamuzi wa kumchukua ni suala la kujiweka katika mazingira magumu.