Ronaldo afunika kila kona Real Madrid

Muktasari:

Ronaldo anaongoza kwa kufunga katika mashindano hayo akiwa na mabao 15, lakini ndiye mchezaji aliyekimbia umbali mrefu zaidi katika mechi 10 alizoichezea Real hadi sasa.

Madrid, Hispania. Ligi ya Mabingwa ndiyo mashindano yanayoonyesha ubora wa mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

Ronaldo anaongoza kwa kufunga katika mashindano hayo akiwa na mabao 15, lakini ndiye mchezaji aliyekimbia umbali mrefu zaidi katika mechi 10 alizoichezea Real hadi sasa.

 

Ronaldo amecheza mechi zote za Ligi ya Mabingwa msimu huu akiwa amekimbia umbali wa kilomita 92 na mita 142.

 

Kwa kuongeza hilo la kasi yake Ronaldo amekuwa akikimbia kwa kasi ya kilomita 31 kwa saa.

 

Anayemfutia Ronaldo ni Casemiro kiungo huyo amekimbia kilomita 90 katika michezo tisa hasi sasa.

 

Nafasi ya tatu inachukuliwa na kiungo Toni Kroos, aliyekimbia umbali wa kilomita 86.349, ndani ya  dakika 682.

 

Wachezaji 10 waliokimbia umbali mrefu Real Madrid katika mashidano ya Ligi ya Mabingwa ni

1: Cristiano Ronaldo: mechi 10, dakika 900, Km92.142

2: Casemiro: mechi 9, dakika 755, 89.762 km

3: Toni Kroos: mechi 9, dakika 682, 86.349 km

4: Sergio Ramos: mechi 8, dakika 720, 79.632 km

5: Isco: mechi 9, dakika 630, 79.126 km

6: Luka Modric: mechi 8, dakika 688, 75.025 km

7: Marcelo: mechi 8, dakika 688, 73.037 km

8: Raphael Varane: mechi 8, dakika 668, 72.705 km

9: Dani Carvajal: mechi 6, dakika 540, 62.784 km

10: Nacho: Mechi 6, dakika 540,  57.806 km