Ronaldo ajivunia rekodi ya Real kwa PSG

Tuesday February 13 2018

 

Madrid, Hispania. Cristiano Ronaldo amekiri kuwa Real Madrid inahitaji kuwa katika ubora wake ili kuifunga Paris Saint-Germain katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa utakaochezwa kesho Jumatano.
Ronaldo alisema hayo baada ya kuifunga mabao matatu Real Sociedad katika ushindi wao wa mabao 5-2 mwishoni mwa wiki.
Mreno huyo hivi karibuni alipewa tuzo yake ya Goal 50 Award iliyomfanya kuwa mchezaji bora wa msimu uliopita 2016/17.
"Tunakwenda kucheza dhidi ya timu bora yenye wachezaji wazuri, lakini tunatakiwa kuonyesha kuwa Real Madrid ni timu inayoundwa na wachezaji wenye uzoefu," alisema Ronaldo.
"Tunatakiwa kuwa makini katika mechi hizi mbili muhimu na kuhakikisha tunasonga mbele katika Ligi ya Mabingwa.
"Tunawaheshimu PSG, lakini sisi ni wamoja na tumejiandaa kwa lolote."