Real yataka euros100 mil kuwatoa Morata, Danilo

Muktasari:

Bado kuna sintofahamu ndani ya Santiago Bernabeu kuhusu wachezaji hao wawili, ambao Zinedine Zidane anataka kuendelea kuwa nao katika kikosi hicho.

Madrid, Hispania. Kama Alvaro Morata na Danilo watauzwa wiki hivi karibuni, Real Madrid inategemea kupata si chini ya euros 100 milioni.

Bado kuna sintofahamu ndani ya Santiago Bernabeu kuhusu wachezaji hao wawili, ambao Zinedine Zidane anataka kuendelea kuwa nao katika kikosi hicho.

Huku Karim Benzema akiwa bado ni chaguo la kwanza mbele ya Morata naye chipukizi Dani Carvajal akionekana kuchukua nafasi ya Danilo.

AC Milan inaendelea kufuatilia kwa karibu nyota huyo kwa kutoa euros 70milioni, dau ambalo linaweza kuongezeka, wakati Chelsea nayo ikiwa haijatoa neno lake la mwisho kuhusu suala hilo.

Danilo anategemea kutua Stamford Bridge, kama siyo Manchester City iliyoweka bayana dau la euros 30 milioni.