Real Madrid yamfungia vioo Ronaldo

Muktasari:

Ronaldo ameinunia timu yake baada ya kushindwa kumuongezea pesa katika mkataba ambapo anataka kuwa sawa na staa wa Barcelona, Lionel Messi pamoja na staa wa PSG, Neymar huku akiamini Madrid imemsaliti.

REAL Madrid imeamua kumfungia milango staa wake, Cristiano Ronaldo na haijali madai yake ya kutaka kuondoka katika dirisha hili kubwa la uhamisho huku ikiwa tayari kumruhusu staa huyo kutimka Santiago Bernabeu.

Ronaldo ameinunia timu yake baada ya kushindwa kumuongezea pesa katika mkataba ambapo anataka kuwa sawa na staa wa Barcelona, Lionel Messi pamoja na staa wa PSG, Neymar huku akiamini Madrid imemsaliti.

Hata hivyo, Madrid haipo tayari kumuongezea pesa zaidi staa huyo ambaye anaelekea ukingoni na ipo tayari kumuona akiondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka tisa tangu alipowasili mwaka 2008 akitokea Manchester United.