Rais wa Shirikisho la Soka Hispania mbaroni kwa matumizi mabaya ya fedha za ofisi

Muktasari:

Villar ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Hisapania, amekuwa Rais wa Shirikisho hilo tangu mwaka 1988.

Hispania. Rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Angel Villar  pamoja na mtoto wake wa kiume, Gorka wanashikiliwa na polisi kutokana na kutuhumiwa kufuja fedha na matumizi mabaya ya madaraka.

Villar ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Hisapania, amekuwa Rais wa Shirikisho hilo tangu mwaka 1988.

Watuhumiwa hao wametiwa mbaroni leo Jumanne, huku Mahakama Kuu nchini humo kupitia Kitengo cha Uchunguzi na Makosa ya Rushwa kikiendelea kukusanya ushahidi.

Mtoto wa kiongozi huyo ni miongoni mwa watu waliounganishwa kwenye mashataka hayo.

Villar anatuhumiwa kufuja fedha kupitia mpango wa kuandaa mechi za kimataifa za kirafiki. Hata hivyo  mawakili wa Villar hawajazungumza jambo lolote kuhusiana na tuhuma hizo zinazomkabili.