Pogba amshukuru Neymar kwa penalti

Muktasari:

  • Ukweli kuwa, Pogba alikimbia kama alivyofanya 2011 wakati Man United akademi ilipocheza na Liverpool katika robo fainali ya Kombe la FA kwa vijana.

London, England. Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amemshukuru Neymar kwa kumsaidia kufunga penalti dhidi ya Leicester City Ijumaa iliyopita.
Pogba (25) alijifunza mbinu ya kupiga penalti hiyo kutoka kwa Neymar miaka nane iliyopita walipokuwa timu za vijana.
Ukweli kuwa, Pogba alikimbia kama alivyofanya 2011 wakati Man United akademi ilipocheza na Liverpool katika robo fainali ya Kombe la FA kwa vijana.
Man United ikiwa nyuma kwa mabao 2-0, Pogba alichukua uamuzi wa kupiga penalti mbele ya mashabiki 15,000 wa Liverpool pamoja na Sir Alex Ferguson.
Akiwa mwenye kujiamini, Mfaransa huyo wakati huo akiwa na miaka 18 tu, alipiga penalti hiyo na kufunga kabla ya kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano.
Pogba alirudia tena mbinu hiyo Ijumaa wakati alipopiga penalti hiyo na kumwacha kipa Kasper Schmeichel anayesifika kwa kuokoa penalti asijue la kufanya katika ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester.