Ozil amtibua Wenger upyaa

Tuesday November 14 2017

 

LONDON, ENGLAND. Atletico Madrid wameibuka wakiwa na lengo la kumuudhi kocha wa Arsenal, Arsene Wenger!  Wanamtaka  Mesut Ozil lakini bure.
Klabu hiyo inamshawishi mchezaji huyo asikubali kusaini mkataba wake mpaka Januari ili wampe mkataba wa awali na kisha mnamo Juni wamchukue bure.
 Mkataba wa Ozil utaisha mwishoni mwa msimu dalili ya kuondoka akiwa huru ni kubwa.
Arsenal imekuwa ikijaribu kumshawishi mchezaji huyo asaini mkataba mpya bila mafanikio na uongozi wa klabu hiyo haupo tayari kumtoa bure kwa kuwa walimnunua kwa pesa nyingi, yaani Pauni 42.5 milioni mwaka 2013 kutoka Real Madrid.
Bosi wa Atletico, Diego Simeone amepeleka moto Arsenal hasa baada ya kumwambia Ozil kwamba atamlipa kiasi cha Pauni 200,000 kwa wiki.