Nyota wawili wamvalia njuga Pogba arudi Juventus

Muktasari:

  • Wachezaji wawili ambao ni marafiki zake, Blaise Matuidi na Paulo Dybala wamekuwa kwenye ushawishi mkubwa kwa nyota huyo aliyeingoza Ufaransa kutwaa taji la Kombe la Dunia, katika mchezo uliopigwa Jumapili iliyopita, huku wakiidhibu vikali Croatia kwa mabao 4-2.

Nyota wa Manchester United, Paul Pogba huenda hatima yake ya kuendelea kubaki kwenye klabu yake ya sasa ipo njiapanda kutokana na uhusiano usioridhisha na Kocha Jose Mourinho, huku mchezaji huyo akishawishiwa na wachezaji wa Juventus kuwa arudi kwenye klabu yake ya zamani.
Wachezaji wawili ambao ni marafiki zake, Blaise Matuidi na Paulo Dybala wamekuwa kwenye ushawishi mkubwa kwa nyota huyo aliyeingoza Ufaransa kutwaa taji la Kombe la Dunia, katika mchezo uliopigwa Jumapili iliyopita, huku wakiidhibu vikali Croatia kwa mabao 4-2.
Pobga anatajwa kuwa huenda akahama Man United kutokana na msimu uliopita kutokuwa na uhakika wa namba mbele ya kocha Mourinho.
Nyota huyo mwenye miaka 25, amefanikiwa kuonyesha kwenye uwezo wake kwenye Kombe la Dunia kuwa kwa nini Man United ilimsajili kwa dau la Pauni 89 milioni.