Neymar kukaa jukwaani

Friday September 8 2017

 

PARIS, UFARANSA. Paris Saint-Germain ina mpango wa kumpumzisha Neymar Jr. kwenye mechi dhidi ya  Metz leo usiku, wakilenga kumpa nafasi ya kupumzika tayari kwa kupambana na Celtic kwenye kipute cha Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne wiki ijayo.
 Neymar alicheza mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia  Jumatatu wiki hii akiwakilisha timu yake ya Brazil dhidi ya Colombia sambamba na wachezaji wenzake wa PSG Marquinhos, Dani Alves na Thiago Silva.
Wachezaji hao walirudi uwanjani Jumatano wiki hii na kocha Unai Emery huenda akawapumzisha baadhi kwenye mechi hiyo ya Ligue 1 itakayofanyika Stade Saint-Symphorien.
Hata hivyo Thiago Silva huenda asicheze mechi ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa wakati Angel Di Maria naye ameumia misuli.