Napoli waijadili Manchester City

Muktasari:

Manchester City imekuwa na rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye mechi zake za hivi karibuni jambo ambalo limewafanya Napoli kujitutumua kwamba hawaihofii timu hiyo ya England.

Italia. Kocha wa Napoli, Maurizo Sarri amesema kikosi chake kitaonyesha umafia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City leo Jumanne.
Napoli na Manchester City zote zinaongoza kwenye ligi za nchini mwao, lakini Manchester City wamejiwekea rekodi ya  kushuka dimbani na kutoa kipigo kikali jambo ambalo linahofiwa linaweza kujitokeza kwa Napoli.
Kocha Sarri alisisitiza kwamba kikosi chake kinashuka leo uwanjani bila kuwa na hofu yoyote licha ya rekodi nzuri waliyonayo City kwenye EPL.