Neymar, Griezmann kumaliza ubabe wa Ronaldo, Messi

Muktasari:

Wengi wamekaribia lakini hakuna aliyefanikiwa kushinda tuzo hiyo.

Paris, Ufaransa. Ni muda mrefu umepita tangu Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekuwa wakipokezana kutwaa tuzo ya Ballon d'Or, wakati tunaelekea mwaka 2018 swali limebaki ni nani wa kuvunja utawala huo?
Wengi wamekaribia lakini hakuna aliyefanikiwa kushinda tuzo hiyo.
Wesley Sneijder mwaka 2010 alishika vichwa; huku Antoine Griezmann alikuwa na nafasi nzuri 2016, lakini alishindwa baada ya kukosa kuiongoza Ufaransa kutwaa ubingwa wa mataifa ya Ulaya.
Wakati wawili hao Messi, Ronaldo wameanza kuzeeka, kumeanza kutoa mwanya kwa majina mengine kuchomoza katika kuwania tuzo hiyo.


Neymar
Kama kuna mchezaji anayepewa nafasi kubwa ya kumaliza ufalme wa nyota hao wawili basi ni Neymar.
Katiak mwaka wa Kombe la Dunia akiendelea kucheza kwa kiwango chake alichoanza nacho Paris Saint-Germain akiwa na wachezaji wenzake na kufanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu hakuna ubishi taji litakwenda kwake.


Mbappe
Ukianga kiwango cha chipukizi huyo wa Ufaransa hakuna shaka kama naye anastahili kuingia katika kinyang’anyiro hicho cha kuwania Ballon d'Or.
Bado ni kijana mdogo lakini kipaji chake kimeanza kutikisa kiasia cha Mbappe kufaninisha kuwa ni Thierry Henry mapya.


Isco
Isco haitaji tena kusubiri kuthibisha ubora wake, amekuwa na mchango mkubwa Real Madrid kwa kuwa moja ya wachezaji tegemeo ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Hispania ikiwa imefuzu kwa Kombe la Dunia Russia, itakuwa nafasi yake nyingine ya kuthibisha ubora wake katika kikosi cha kocha Julen Lopetegui, kama akiongoza timu yake ya taifa kufunya vizuri hakuna shaka nyota huyo zamani Malaga ataingia kati vita hiyo.


Hazard
Akiwa na miaka 26, Eden Hazard tayari ameshinda tuzo ya mchezaji bora Ligue 1 na mchezaji bora wa Ligi Kuu England.
Hiyo ni wazi imeonyesha kuwa ni moja ya wachezaji wanaostahili kuwapokea kijiti cha Messi na Ronaldo kuanzia mwakani.
Griezmann
Baada ya kuikaribia 2016, Griezmann amepoteza makali yake mwaka huu, japokuwa anayo nafasi ya kurudi upya wakati wa Kombe la Dunia atakapoingoza Ufaransa kusaka ubingwa huo.
Hiyo ni nafasi yake ya pekee baada ya kuanza vibaya msimu na atathibisha ubora wake Juni mwakani.

De Bruyne
Kiungo huyo Mbelgiji amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Manchester City msimu huu chini ya kocha Pep Guardiola.
Amekuwa akicheza kama kiungo wa kati, amerudi katika ubora wake akiwa na rekodi ya kutegeneza pasi za mabao 33 tangu alipojiunga na City. Mafanikio hayo akionyesha katika Kombe la Dunia basi naye atakuwa kati ya wachezaji wanaoweza kunyakuwa tuzo hiyo mwakani.
Kiungo huyo Mbelgiji amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Manchester City msimu huu chini ya kocha Pep Guardiola.
Amekuwa akicheza kama kiungo wa kati, amerudi katika ubora wake akiwa na rekodi ya kutegeneza pasi za mabao 33 tangu alipojiunga na City. Mafanikio hayo akionyesha katika Kombe la Dunia basi naye atakuwa kati ya wachezaji wanaoweza kunyakuwa tuzo hiyo mwakani.