Mwingereza Johana Konta kukutana na Mmarekani Venus William nusu fainali tenisi Webledon 2017

Thursday July 13 2017

 

London, England. Mcheza tenisi Johana Konta (26) amemfunga Mromania, Simona Halep na kufanikiwa kutinga nusu fainali ya mashindano ya Wembledon 2017.

Konta alitumia saa mbili na dakika 38 kumuondoa mpinzani wake hivyo kutinga nusu fainali mchezo ambao atakutana na Mmarekani, Venus Williams.

 Konta alisema wakati wote amekuwa akijiamini hivyo anaamini ndoto zake zitatimia kwa kumfunga mpinzani wake kwenye mchezo wa nusu fainali.

Mwingereza Konta ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kutinga nusu fainali ya mashindano hayo, ikiwa ni ni tangu mwaka 1977 ambapo Dwyane Wade alinyakua taji hilo.