Mwanariadha afariki dunia akiwa mazoezini mashindano ya Dunia ya Walemavu London

Thursday July 13 2017

 

London, England. Mwanariadha raia wa Nchi za Falme za Kiarabu, Abdullah Hayayei amefariki dunia ghafla wakati akiwa mazoezini  wakati akijiandaa na Mashindano ya Dunia ya Walemavu yanayoendelea London, Uingereza.

Gari la wagonjwa lilifika muda mfupi baada ya kutolewa taarifa kuwa alikuwa amepata majeraha wakati akiwa mazoezi.

Baada ya madaktari kuthibitisha kifo chake, ndugu zake walitaarifiwa tukio hilo,  jambo ambalo liliwashtua.

Mashindano hayo ya Walemavu ya Dunia yaliyofanyika mjini Rio mwaka 2016, Hayayei alimaliza katika nafasi ya sita.