Shabiki wa Chelsea adaiwa kumtwanga mwamuzi kwa chupa ya bia

Muktasari:

Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita kwenye uwanja wa Selhurst Park ambako Chelsea ilichezea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

England. Polisi nchini Uingereza imeanzisha uchunguzi wa wazi kubaini shabiki aliyetupa chupa ya pia uwanjani na kumpiga mwamuzi msaidizi, Sian Massey-Ellis.
Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita kwenye uwanja wa Selhurst Park ambako Chelsea ilichezea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Mwamuzi huyo alikutana na kadhia hiyo wakati akitekeleza majukumu yake uwanjani huku alipokuwa akikimbia na kupita eneo ambalo walikuwapo mashabiki wa Chelsea.
Hivyo polisi wameanza kufuatilia kamera zilizokuwapo uwanjani hapo ili kubaini muhusika wa tukio hilo.