Mtoto wa Sunderland aagwa kishujaa

Friday July 14 2017

 

London, England. Maelfu ya waombolezaji walijitokeza kumuaga kwa heshima mtoto Bradley Lowery (6), aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na matatizo ya saratani.

Wachezaji mbalimbali walijitokeza kumuaga marehemu Bradley, huku mshambuliaji wa zamani wa Sunderland, Jermain Defoe akishindwa kujizua na kumwaga machozi.

Defoe alijenga urafiki na mtoto huyo mara baada ya kugundulika kwa tatizo lake la kansa.

Misururu ya watu ilimiminika mitaani wakati mwili huo ukipelekwa kanisani kwa ajili ya ibada ya mazishi.