Messi, Ronaldo wamchanganya mtangazaji Ulaya

Muktasari:

Mtangazaji huyo alitoa kauli hiyo wakati akifanya tathmini ya wachezaji hao wawili kwenye kipindi cha Aky Sports News akisisitiza kwamba kuna sababu moja tu ambayo labda naweza kuamua ni nani bora kati ya nyota hao wawili.

England. Mtangazaji Natalie Sawyer amesema ameshindwa mpaka sasa kubaini tofauti ya ubora kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Mtangazaji huyo alitoa kauli hiyo wakati akifanya tathmini ya wachezaji hao wawili kwenye kipindi cha Aky Sports News akisisitiza kwamba kuna sababu moja tu ambayo labda naweza kuamua ni nani bora kati ya nyota hao wawili.
Alisema wakati unamwangalia Messi labda utumia kigezo  yule ambaye wakati huo anakuwa kwenye chati, vilevile ndivyo ilivyo kwa Ronaldo.
Wachezaji hao wawili wote wana tuzo tano za Ballon d’Or ambapo Ronaldo alisherehekea tuzo yake hiyo ya wiki iliyopita.