Mshahara wamchelewesha Barkley kutua Spurs

Muktasari:

Staa huyo wa Everton, Barkley amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua Spurs, lakini matakwa yake ya kutaka alipwe mshahara mkubwa ndicho kinachochelewesha dili hilo kukamilika hadi sasa.

Kiungo Ross Barkley ameripotiwa kwamba anataka kulipwa mshahara mkubwa kuliko anaolipwa Harry Kane katika kikosi cha Tottenham Hotspur kwa sasa.

Staa huyo wa Everton, Barkley amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua Spurs, lakini matakwa yake ya kutaka alipwe mshahara mkubwa ndicho kinachochelewesha dili hilo kukamilika hadi sasa.

Kane analipwa Pauni 120,000 kwa wiki, lakini Barkley anataka alipwe Pauni 150,000 kwa wiki.