Mourinho awavamia Lewandowski na Thiago

Muktasari:

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho hana msaidizi wa staa wake, Romelu Lukaku tangu kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic na amekuwa akimtaka Lewandowski ambaye tayari alishaelezea nia yake ya kuondoka Allianz Arena.

MANCHESTER United inafikiria kuivamia kambi ya Bayern Munich na kuwatwaa mastaa wawili wa timu hiyo, mshambuliaji, Robert Lewandowski na kiungo mahiri mchezeshaji, Thiago Alcantara kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho hana msaidizi wa staa wake, Romelu Lukaku tangu kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic na amekuwa akimtaka Lewandowski ambaye tayari alishaelezea nia yake ya kuondoka Allianz Arena.

Kwa upande wa Thiago, inasemekana staa huyo amedhamiria kurudi katika klabu yake ya zamani wa Barcelona, lakini Mourinho anamtaka kwa ajili ya kutengeneza ufundi katika eneo la mwisho baada ya kukosa mchezaji wa aina yake msimu uliopita.