Mourinho awageukia Lukaku, Fellaini

Muktasari:

Man United ilitwaa Kombe la FA, baada ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Wembley.

London, England. Jose Mourinho amesema,  hakufurahishwa na Romelu Lukaku na Marouane Fellaini kuweka ngumu na kushindwa kucheza mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea.

Man United ilitwaa Kombe la FA, baada ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Wembley.

Wakati Lukaku alidai ana jeraha la kifundo cha mguu na Fellaini alikosa mechi tatu kutokana na majeraha ya misuli kabla ya mchezo huo wa Jumamosi.

Hata hivyo, inadaiwa wachezaji hao wa timu ya Taifa ya Ubelgiji walidai ni wagonjwa na walihofia kuumia hatua ambayo ingewakosesha fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Juni 14 nchini Russia.

Chanzo cha karibu kilidokeza wachezaji hao walijumuishwa katika kikosi ambacho kingeivaa Chelsea kabla ya kuenguliwa muda mfupi.