Mourinho amtega Carrick kikosi cha kwanza

Muktasari:

Carrick leo Jumatano anatazamiwa kuanza pambano la kwanza msimu huu dhidi ya Burton katika michuano ya kombe la Ligi na Mourinho amedai kwamba Carrick anaweza kuitumia michuano hiyo kuonyesha jinsi anavyostahili kuanza katika kikosi cha kwanza cha United katika michuano mingine.

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amedai kwamba kiungo wake mkongwe, Michael Carrick anaweza kupambana na kuhakikisha anarudi tena katika kikosi cha kwanza baada ya kushindwa kufanya hivyo katika mechi sita za kwanza za Ligi Kuu ya England.