Real Madrid wahaha kumnasa David de Gea

Muktasari:

Mwaka 2015 kulikuwa natetesi nyingi kwamba mchezaji huyo angejiunga na Real Madrid lakini baadaye mpango ukashindikana katika dakika za mwisho.

MANCHESTER England. TAARIFA kutoka Real Madrid zinasema kuwa klabu hiyo inataka kuhakikisha David de Gea anatua Hispania katika dirisha la usajili linalokuja na mpango ni kutoa kiasi kikubwa cha pesa pamoja na mchezaji mmoja kwa Manchester United.
Mwaka 2015 kulikuwa natetesi nyingi kwamba mchezaji huyo angejiunga na Real Madrid lakini baadaye mpango ukashindikana katika dakika za mwisho.
Sasa Real Madrid wanakuja na kasi nyingine kuhakikisha wanamsajili mchezaji huyo huku wakipanga kumpatia kiasi cha Pauni 200,000 kwa wiki.
Ukweli ni kwamba Manchester United hawapo tayari kupoteza mchezaji mzuri wakati huu ambao wanapambana kwa udi na uvumba na Man City katika mbio za kunyakua ubingwa na ni wazi kwamba kama itabidi kubadilishana wachezaji basi watahitaji wachezaji wenye kiwango cha juu.
Taarifa ni kwamba Man United huenda wakakubali iwapo kipa KeylorNavas ndiye atahusishwa katika mpango huo.