Milner hakamatiki Ulaya Neymar anasubiri

Muktasari:

Milner ameweka rekodi mpya kwa kutoa pasi za usaidizi mara tisa katika mchezo mmoja na kumzima nahodha huyo wa Brazil.

LONDON, ENGLAND. JAMES Milner wa Liverpool, amevunja rekodi ya mshambuliaji wa Paris Saint Germain PSG Neymar katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Milner ameweka rekodi mpya kwa kutoa pasi za usaidizi mara tisa katika mchezo mmoja na kumzima nahodha huyo wa Brazil.

Neymar ambaye ni mchezaji ghali duniani, alikuwa akishika rekodi hiyo mwaka juzi baada ya kutoa pasi za usaidizi mara nane.

Mchezaji huyo amecheza kwa kiwango bora mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao Liverpool ilishinda mabao 5-2.

Mara ya mwisho mchezaji kutoa pasi za usaidizi mara tisa ilikuwa msimu 2003-2004 kabla ya Milner kuifikia juzi usiku.

Mabao mawili ya Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane yalitosha kuipa ushindi mnono Liverpool.

Baadhi ya wachezaji waliowahi kuweka rekodi ni Xavi Hernandez aliyoweka 2008-2009 kwa kutoa pasi mara saba akiungana na Zlatan Ibrahimovic (2012-2013), Ryan Giggs (2006-2007), Mesut Ozil (2010-2011).

Pia wamo Andres Iniesta, Thierry Henry, Ousmane Dembele, Roberto Firmino na Wesley Sneijder waliotoa pasi mara sita kila mmoja.

Milner, ambaye ametangaza kustaafu soka ya kimataifa mwaka juzi amecheza mechi 61 katika kikosi cha England.